Mbunge wa Sirisia John Waluke leo alijisalimisha katika mahakama ya Milimani baada ya jaji wa maakama kuu Esther Maina kudumisha kifungo chake cha miaka 67 gerezani kwa madai ya kuilaghai halmashauri ya nafaka na mazao shilingi milioni 313.
Waluke alijipeleka Mahakama ya Milimani Ijumaa alasiri ambapo alizuiliwa katika seli za chini ya ardhi akisubiri kuhamishwa gerezani.
Waluke na mshirika wake wa kibiashara Grace Wakhungu walipatikana na hatia mwaka wa 2020 na kuhukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Shilingi milioni 297 kupitia mikataba isiyokuwa ya halali katika Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB).
+ There are no comments
Add yours