Serikali Ya Kaunti Ya Kilifi Yasambaza Mbegu Za Mahindi Na Mbolea Kwa Wakulima

Estimated read time 1 min read

Uongozi wa kaunti ya Kilifi ikiongozwa na Gavana Mung’aro imezindua rasmi mpango wa usambazaji wa mbegu za mahindi tani 66 na mbolea bila malipo, zikiwalenga wakulima zaidi ya 11,000 kaunti hiyo. Pembejeo zitasambazwa katika Wadi zote 35 na zimegharimu serikali ya kaunti hiyo kima cha shilingi milioni 100. Lengo ni kusaidia wakulima kuzalisha chakula cha kutosha.

Gavana pia amekiri kuwa kaunti hiyo inakumbwa na changamoto ya tingatinga, mengi yamekuwa katika hali duni na hayawezi kuwafikia wakulima wote, lakini uongozi wake umeweka mpango wa kununua tingatinga mpya na kukarabati baadhi ili ziweze kutoa huduma bora na kwa wakati unaofaa.

Amewahimiza wakulima kuwa na desturi ya kuandaa mashamba yao mapema ili msimu wa mvua ukianza, mashamba yawe tayari kwa upanzi.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours