Hatimaye Chelsea wameweza kutoa machungu yao dhidi ya klabu ya West Ham baada ya kuwacharaza mabao 5 nunge.
Star wa Chelsea Cole Palmer alifungua ukurasa wa mabao kwa daki
Ndani ya dakika 15, Palmer alijibu kwa haraka zaidi mpira uliopigwa na Nicolas Jackson na kupatia Blues bao la kuongoza. Vijana wa Mauricio Pochettino waliongeza mabao mengine mawili kabla ya kipindi cha mapumziko hata hivyo hawakuwahusisha Palmer huku Conor Gallagher na Noni Madueke wakiwa wafungaji.
Nicolas Jackson alifungia chelsea mabao mawili baada ya mda wa mapumziko na kuweza kuwafungia ushindi
+ There are no comments
Add yours