Baada ya kupangua penalti nne (4) na kuivusha Afrika Kusini kwenda hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika 2023, nyanda wa Mamelodi Sundowns, Ronwen Williams amekuwa golikipa wa kwanza kuokoa penalti nne kwenye mechi moja ya AFCON iliyofikia hatua ya MATUTA.
Afrika Kusini imetinga nusu fainali ya AFCON 2023 kufuatia ushindi wa penalti 2-1 dhidi ya Cape Verde na itachuana na ‘The Super Eagles’, Nigeria kwenye hatua hiyo.
Nusu fainali nyingine itawakutanisha wenyeji, Ivory Coast dhidi ya Henock Inonga na wenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
+ There are no comments
Add yours