ALIKIBA ATUPA JIWE “HII SIO MEDIA YA FAMILIA”

Estimated read time 2 min read

Msanii wa Bong flava Ali Saleh Kiba almarufu kama Ali kiba Baada ya uzinduzi wa Radio yake kwa jina #CrownFm akiwa jukwaani akiimba alisema kuwa “Hii sio media ya familia ambayo watu wengi walioajiriwa ni ndugu”

Alikiba amezindua kituo cha redio kwa jina “Crown FM”. Uzinduzi huo ulifanyika usiku wa Jumamosi Machi 9 2024 katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dare es Salaam kwenye sherehe ya miaka 20 ya Kiba katika muziki.

Sherehe ya miaka 20 ya Ali Kiba ilihudhuriwa na viongozi wengi mashuhuri nchini Tanzania akiwemo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Nape Nauye Waziri Wa Habari,Mawasiliano Na Tecknolojia Ya Habari, Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwigulu Chemba ambaye ni Waziri wa Fedha na Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Chalinze.

Wanamuziki wenza walikuwepo pamoja na wajasiriamali mbali mbali nchini Tanzania.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Kiba alielezea kwamba vyombo vya habari ni muhimu ndivyo vimemkuza kama mwanamuziki na anakumbuka alizawadiwa redio ndogo na babake wakati akikua.

Mwimbaji huyo alisema pia kwamba changamoto ambazo amepitia pia zilimpa msukumo wa kuanzisha kampuni ya uanahabari ambayo ina kituo cha redio na cha runinga.

Crown FM ambayo itapeperusha matangazo yake kwenye masafa ya 92.1 FM inapatikana jijini Dar es salaam, kisiwani Zanzibar, Tanga pamoja na eneo la Pwani nchini Tanzania.

Je, unahisi kamaanisha Nini au ujumbe ni wa nani aliposema “Hii Sio Media Ya Familia”?

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours