Brigedia Swaleh Said Azikwa Kikambala, Kaunti Ya Kilifi

Estimated read time 1 min read

Brigedia wa KDF Swaleh Nzaro Said alizikwa leo Ijumaa mwendo wa saa kumi na mbili jioni katika shamba lake huko Kikambala, kaunti ya Kilifi.

Brig Said alikuwa miongoni mwa maafisa wakuu wa kijeshi walioangamia katika ajali ya chopper eneo la Kaben, kaunti ndogo ya Marakwet Mashariki Alhamisi mchana.

Mwili wa Said uliwasili Mombasa katikati ya asubuhi na kupelekwa nyumbani kwa mamake huko Majaoni, kaunti ndogo ya Kisauni kwa maandalizi.

Hapo awali, familia hiyo ilikuwa imepanga kuweka mabaki yake katika nyumba ya mama huyo huko Majaoni lakini ikabainika kuwa alitamani kuzikwa katika shamba alilonunua eneo la Kikambala, Kaunti ya Kilifi.

Alipewa salamu ya bunduki 13.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours