Idara ya Anga nchini Kenya imetangaza kumalizika kwa Kimbunga Hidaya kilitangaza kumalizika baada ya kuanguka kwenye Kisiwa cha Mafia nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Huduma za Hali ya Hewa Dkt David Gikungu katika taarifa anasema mawingu yanayoandamana na Kimbunga Hidaya pia yamedhoofika na kusambaa pande mbalimbali.
Dkt Gikungu hata hivyo anaonya kuwa kuanzia Jumatatu hadi Jumanne, mvua kubwa inayoambatana na upepo mkali itashuhudiwa katika ukanda wa pwani na kuathiri kaunti za Kwale, Mombasa, Kilifi na Lamu.
+ There are no comments
Add yours