MAREKANI – Kamala Tunashinda Asubuhi Sana -Donald Trump

Estimated read time 1 min read

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema pendekezo la Kamala Harris kugombea kiti cha urais cha taifa hilo ni afueni kwake kwa kuwa Rais wa sasa Joe Biden alikuwa na ushawishi na alifanya uchaguzi uwe mgumu.

Akizungumza na CNN baada ya Rais Biden kujitengua katika kinyang’anyiro hicho, Trump amesema Kamala “atakuwa mpinzani rahisi kushindwa kuliko ambavyo ingekuwa kwa Biden.”

Biden alimaliza kampeni yake ya kuchaguliwa tena Jumapili baada ya Wanademokrasia wenzake kupoteza imani kwake na uwezo wake wa kumshinda Trump. Biden alimhidhinisha Harris kuchukua nafasi yake kama mgombea wa chama.
Biden alikabiliwa na mashaka yanayoongezeka juu ya nafasi zake za kuchaguliwa tena baada ya utendaji dhaifu na uliodorora katika mjadala wa televisheni dhidi ya Trump mwishoni mwa mwezi uliopita.
Katika mtandao wake wa Jamii wa The Truth, siku ya Jumapili, Trump alisema Biden “hafai kugombea Urais, na kwa hakika hafai kuhudumu.”

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours