Rais wa Marekani Joe Biden amesema atasimama na Makamu wake wa Rais Kamala Harris kuchaguliwa kuwa mgombea mteule wa Chama cha Demokrati katika uchaguzi wa Novemba.
Rais Biden alitangaza kumuunga mkono Kamala kupitia ukurasa wake wa X, muda mfupi baada ya kutangaza uamuzi wa kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho.
Akirejelea uamuzi wake wa “kutokubali uteuzi” na kuelekeza “nguvu” zake zote kwenye majukumu yake ya urais, Biden alisema kumchagua Harris kama Makamu wake wa Rais ndio “uamuzi bora” aliofanya.
“Leo nataka kutoa usaidizi wangu kamili na kumuidhinisha Kamala kuwa mteule wa chama chetu mwaka huu. Wanademokrasia – ni wakati wa kukusanyika na kumpiga Trump. Wacha tufanye hivi,” Biden aliandika.
Muda mfupi kabla ya kumuidhinisha Harris, Biden alitoa barua ya wazi kutangaza kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha urais.
“Ingawa imekuwa nia yangu ya kutaka kuchaguliwa tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi kwa mimi kujiuzulu na kuzingatia tu kutimiza wajibu wangu kama Rais kwa muda wote uliosalia wa muhula wangu,” aliandika. , akiahidi kulihutubia taifa kuhusu suala hilo baadaye.
+ There are no comments
Add yours