Wakenya 1,000 Wanasafirishwa Kufanya Kazi Nje ya Nchi Kila Wiki – Rais Ruto

Estimated read time 1 min read

Rais William Ruto mnamo Jumapili, Julai 28, alifichua kuwa nchi ilikuwa ikisafirisha raia 1,000 kila wiki kufanya kazi katika mataifa ya kigeni.

Rais alifichua hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Mwatate huko Taita Taveta muda mfupi baada ya ibada ya kanisani.
Ruto alisema kuwa vijana hao wa Kenya walikuwa wakisafirishwa nje ya nchi kupitia kwa uratibu wa mashirika tofauti na wizara ya Leba na Ukuzaji Ujuzi inayoongozwa na Katibu Mkuu (PS) Shadrack Mwadime.

Kulingana na Mkuu wa Nchi, usafirishaji mkubwa wa mtaji wa binadamu ulikuwa mojawapo ya njia ambazo utawala wake ungetatua mzozo wa ukosefu wa ajira.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours