Kylian Mbappe alifunga bao kwenye mechi yake ya kwanza kusaidia Real Madrid kushinda taji la sita la UEFA Super Cup baada ya kuchapa Atalanta 2 – 0 Jumatano usiku katika uwanja wa PGE Narodowy, Warsaw.
Baada ya sare tasa katika kipindi cha kwanza, kiungo wa kati Federico Valverde alifunga bao la kwanza kwa Madrid mnamo dakika ya 59 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Vinicius Junior.
Madrid waliendelea kuongeza nafasi za kufunga na katika dakika 68 Mbappe akatikisa wavu baada ya pasi aliyoandaliwa Jude Bellingham na kumfunga kipa wa Atalanta Juan Musso.
Ushindi wa Madrid ulimhakikishia kocha Carlo Ancelotti kusawazisha kocha wa zamani wa Los Blancos Miguel Munoz na kushinda rekodi ya pamoja ya mataji 14 akiwa kwenye usukani wa klabu hiyo.
+ There are no comments
Add yours