Mwanasiasa wa Mombasa, ambaye pia ni mgombea ubunge wa eneo la Mvita , Ali Mwatsau, ashambuliwa na risasi katika eneo la Tudor, Mombasa.
Mwanasiasa huyo wa Mombasa Ali Mwatsau alinusurika kuuawa baada ya kupigwa risasi 22 na genge la wahalifu .
Polisi mjini Mombasa wanasema hawajui nia ya kushambuliwa kwa Ali Mwatsau ambaye ni mgombea Ubunge wa Mvita kwa tikiti ya UDA ila bado wanachunguza kisa hicho
Ali Mwatsau alikuwa akitoka msikitini alipovamiwa na watu wasiojulikana na kumiminiwa risasi 22.
+ There are no comments
Add yours