Aliyekuwa mchezaji wa mpira wa klabu ya Everton, Wayne Rooney, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Ligi Kuu ya Soka ya DC United.
Hiyo ni kazi ya pili ya Rooney katika uongozi baada ya kuondoka Derby County mwezi uliopita .
Mfungaji huyo bora wa mabao wa team ya taifa ya uingereza na Manchester United alikaa miezi 18 akiwa na DC United na kuwa nahodha wa timu hiyo kabla ya kujiunga na Derby kama kocha Januari 2020.
Rooney aliendelea kuinoa klabu hiyo katika kipindi ambacho walikuwa kwenye utawala na alikuwa akiiongoza huku wakishushwa daraja hadi Ligi ya Kwanza msimu uliopita.
Timu ya DC United imekuwa bila meneja tangu Aprili. Kocha mkuu wa muda Chad Ashton atasalia kuinoa timu hiyo hadi Rooney atakapopokea viza yake ya kazi.
+ There are no comments
Add yours