Aliyekuwa gavana wa Mombasa Hassan Joho siku ya leo alipeana mamlaka rasmi kwa mrithi wake Abdulswamad Nassir.
Joho alihudumu kwa mihula miwili tangu kuchukua uongozi wa kaunti hiyo mwaka wa 2013 kama gavana wa kwanza kupitia tikiti ya chama cha ODM.
Abdulswamad Nassir ameapishwa kuwa gavana wa pili wa Mombasa. Nassir sasa anachukua nafasi kutoka kwa Hassan Ali Joho ambaye aliongoza kaunti hiyo kwa miaka kumi.
Nassir aliapishwa afisini pamoja na naibu wake Francis Foleni Thoya katika hafla iliyofanyika katika bustani ya Mama Ngina Waterfront. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa Azimio wakiongozwa na kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua na mkuu wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka.
Nassir alihudumu kama mbunge wa Mvita kwa miaka kumi kabla ya kuwania ugavana
+ There are no comments
Add yours