Kizaazaa Mahakama ya Malindi baada ya mwanaume wa umri wa miaka 68 kulilia kucheleweshwa kwa haki

Estimated read time 2 min read

Kizaazaa kiliweza kushuhudiwa katika mahakama ya Malindi siku leo tare 19 Oct, baada ya mwanamume anayekabiliwa na mashtaka ya ulaghai alipoanza kupiga kelele kwa madai ya kuwa mahakama imechelewesha kesi.

Carlos Taka, 68, alidai ya kuwa mahakama ya Malindi ndio mahakama isiyofaa zaidi duniani.

Carlos anashtakiwa kwa makosa sita ya kujipatia pesa kwa kujifanya kuwa afisa wa umma.

Kizaazaa hicho kilichochewa na uamuzi wa hakimu kuahirisha kesi yake kwa mara ya kumi na moja.

“Nimekaa rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa sababu tu baadhi ya mashahidi walishindwa kutoa ushahidi. Hii ndiyo mahakama isiyo na manufaa yoyote duniani,” alisema na kubainisha kuwa haki inayocheleweshwa ni sawa na kunyimwa haki.

Juhudi za Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Malindi, Olga Onalo za kumtuliza zilikwama huku Carlos akiendelea kupiga kelele kwa hasira na kuamsha vicheko kutoka katika chumba cha mahakama kilichojaa watu. Carlso alishangaa ni kwa nini kesi yake ilichukuwa muda mrefu kukamilika ilhali mashahidi wanaishi karibu na mahakama.

Alisema shahidi mmoja anakaa nyuma ya mahakama huku mwingine akiishi eneo la Kwa Ndomo, umbali mfupi kutoka mahakamani.

Awali, mshtakiwa alimuuliza shahidi mmoja maswali na alikuwa akitarajia mashahidi wengine watoe ushahidi ndipo alipojulishwa kwamba hakuna shahidi mwingine.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo akisema ni ahirisho la mwisho na kuuagiza upande wa mashtaka umpeleke shahidi huyo mahakamani.

Hakimu alipanga tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo Desemba 14.

๐™„๐™ก๐™ž ๐™ ๐™ช๐™ฅ๐™–๐™ฉ๐™– ๐™๐™–๐™—๐™–๐™ง๐™ž ๐™ฏ๐™š๐™ฉ๐™ช ๐™ ๐™ฌ๐™– ๐™๐™–๐™ง๐™–๐™ ๐™– ๐™Ÿ๐™ž๐™ช๐™ฃ๐™œ๐™š ๐™ฃ๐™– ๐™˜๐™๐™–๐™ฃ๐™ฃ๐™š๐™ก ๐™ฎ๐™š๐™ฉ๐™ช ๐™ฎ๐™– ๐™๐™š๐™ก๐™š๐™œ๐™ง๐™–๐™ข๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Bonyeza

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours