Hatua hiyo inatokana na Serikali ya Tunisia kudaiwa kuingilia masuala ya soka
Onyo hilo linakuja baada ya maoni ya mara kwa mara kutoka kwa Waziri wa Vijana na Michezo wa Tunisia, Kamel Deguiche, kuhusu uwezekano wa “kuvunja ofisi za shirikisho”.
Fifa inachukulia kauli yake kama jaribio la kuingilia uendeshaji wa shirikisho la soka nchini humo (FTF), na imelitaka shirikisho hilo kutoa ufafanuzi kuhusu majaribio ya kuingilia masuala yake ya ndani na vitisho vya kuvunja ofisi yake.
Ikiwa FIFA itachukua hatua, inaweza kumaanisha kuifungia timu ya taifa ya Tunisia kushiriki Kombe la Dunia la Qatar 2022, ambalo litaanza Novemba 20. Tunisia kwa sasa iko Kundi D pamoja na Denmark, Australia na Ufaransa.
+ There are no comments
Add yours