Mtoto wa Mwimbaji wa Nigeria Davido Afa Maji Kwenye Dimbwi la Kuogelea

Estimated read time 1 min read

Ifeanyi(3) mtoto wa kiume wa Davido na mchumba’ke Chioma afariki dunia baada ya kuzama katika swimming pool katika nyumba yao huko Banana Island

Ifeanyi ambaye alizaliwa mwaka wa 2019 alisemekana kuwa chini ya maji kwa muda mrefu kabla ya kukimbizwa hospitalini lakini kwa huzuni alithibitishwa kufariki alipofika.

Kabla, Davido na Chioma walikuwa wamesafiri kwenda mji wa Ibadani kwa ajili ya tukio la kifamilia na kumuacha mtoto wao na wasaidizi wa hapo ndani na haijajulikana ilifikaje katika swimming pool, kuzama kisha kufariki

Pia imeelezwa watu wengine waliokuwa hapo nyumbani kwa Davido wameitwa polisi kwa mahojiano kuhusu tukio hilo ambalo limemuacha Davido na Chioma katika taharuki ya majonzi

Ukiacha mtoto wa Davido, miaka michache iliyopita nae D’banj msanii maarufu Nigeria, mtoto wake pia alifariki kwa kuzama katika swimming pool

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours