Wakaazi kadhaa waliripoti kujeruhiwa baada ya jengo la ghorofa kuporomoka katika eneo la Marikiti mjini Mombasa.

Estimated read time 1 min read

Jengo moja katika eneo la Marikiti kaunti ya Mombasa liliporomoka mnamo Jumamosi, Mei 27, baada ya kupata nyufa.

Taarifa zilieleza kuwa wakazi kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali huku shughuli za uokoaji zikiendelea katika tukio hilo lililotokea dakika chache saa 1:00 usiku.

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir alikuwa katika eneo la tukio pamoja na maafisa wengine wa dharura na maafisa wa polisi.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours