Nay Wa Mitego Afungiwa Shows Na BASATA

Estimated read time 1 min read

Msanii wa Hip hop nchini Tanzania, Emmanuel Elibarick maarufu kama Nay wa Mitego, amelalamika kunyimwa kibali na Basata cha kufanya show yake Makambako akitaja sababu za wito huo kuwa ni wimbo wake mpya wa ‘AMKENI’.

Katika ‘post’ yake Nay ameandika;

“Nimepokea Barua Ya Wito Leo Asubuhi Kutoka baraza La Sanaa Tanzania #Basata Ikiniitaji Kufika Ofisi Za Basata Leo Saa Nne Asubuhi. Isue Ni Wimbo Wangu Wa #Amkeni Nimeshindwa Kufika Leo Coz Nipo Safarini, Mwanasheria Wangu Amesha fanya Mawasiliano Nao Kuomba Siku Nyingine.

Nay ameweka wazi kuwa alihitajika kufika leo Julai 27, 2023 saa nne asubuhi ila hakuweza kwani yuko safarini.

Kwa mujibu wa ‘post’ yake, msanii huyo hakuweza kuitikia wito kutokana na kuwepo safarini, na badala yake mwanasheria wake ndiye amefanya mawasiliano na baraza akiomba mteja wake afike siku nyingine.

Hivi karibuni msanii huyo ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Amkeni’ akigusia mijadala mtambuka inayoendelea kwa sasa nchini huku kwa sehemu kubwa akiikosoa vikali Serikali iliyopo madarakani kwa sasa.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours