EACC Yaagiza Kusimamishwa Kwa Zabuni ya Mfumo Mpywa Wa Mapato Kilifi

Estimated read time 1 min read

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imeagiza Serikali ya Kaunti ya Kilifi kusimamisha malipo yaliyopangwa ya Sh103.8 milioni kwa ununuzi wa mfumo wa usimamizi wa ukusanyaji mapato.

Katika barua iliyotumwa Jumatatu, Meneja wa EACC katika eneo la Upper Coast, Ben Murei, alimshauri Gavana Gideon Mung’aro kusitisha mchakato wa ununuzi la sivyo akabiliwe na vikwazo kwa ufujaji wa pesa za umma.

Shirika la kupambana na ufisadi lilisema uchunguzi wa awali umegundua ukiukwaji mkubwa wa sheria, na kesi za kupuuza moja kwa moja maslahi ya umma.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours