Raila Odinga Amkosoa Ruto Kwa Msimamo Wake Dhidi Ya Vita Vya Israel Na Palestine

Estimated read time 1 min read

Raila Odinga ametofautiana na msimamo wa rais wa Kenya William Ruto kuhusu mzozo huo na kumshauri kutosalia kimya dhidi ya dhulma kwa Wapalestina.

Rais William Ruto alikuwa mmoja wa viongozi wa ulimwengu kusimama na Israel kufuatia uvamizi wa Oktoba 7.

“Nikiwa hapa Mombasa, nataka kutoa ushauri kwa bwana Netanyahu, Netanyahu, Netanyahu, wacha kuua watoto wakiarabu wa Palestine,” Raila amesema.

“Lazima tulaani kwa maneno makali iwezekanavyo, ukatili uliokosa ubinadamu ambao watoto na wanawake wasio na hatia, wananyanyaswa na utawala wa Netanyahu. Ni unyama,” Raila Odinga ameongeza.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours