Bruno Fernandes Anatakiwa Saudi Arabia Majira Ya Joto

Estimated read time 1 min read

Inaripotiwa kuwa klabu mbalimbali kutoka Nchini Saudi Arabia, zimevutiwa na nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, na inaelezwa kuwa wawakilishi kutoka PIF, “wamiliki wa klabu za Al Hilal, Al Nassr, Al Ahli na Al Ittihad” wanajiandaa kufanya mazungumzo na wakala wa kiungo huyo juu ya uwezekano wa kumsajili msimu ujao.

Habari za hivi punde zinadai kuwa PIF ya Saudi ‘tayari inachukua hatua madhubuti’ kabla ya dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi.

Iwapo uhamisho wa kiungo huyo mwenye miaka 29 kwenda Saudia utakamilika, basi atajiunga na wachezaji wengine wengi kama, Cristiano Ronaldo, Sadio Mane, Karim Benzema na Riyad Mahrez waliojiunga kutokea Ligi Kuu England.

Timu za Saudia pia zinawafuatilia kwa ukaribu winga wa Liverpool, Mo Salah pamoja na Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours