Afueni Kwa Wananchi Baada Ya Serikali Ya Kaunti Ya TaitaTaveta Kusitisha Ujenzi Wa Nyumba Za Magereza

Estimated read time 1 min read

Serikali ya Kaunti kupitia wizara ya Ardhi na Mipangilio,Nishati na Madini imesitisha shughuli za kuanzisha ujenzi wa nyumba za idara ya magereza kwenye ardhi ambayo iko na utata wa umiliki,eneo la Ore,wadi ya kaloleni .

Kwenye kikao na wanachi hii Leo kwenye ardhi hiyo yenye utata ,waziri wa ardhi Elizabeth Mkongo,ameelezea maskitiko yake kufuatia hatua ya kufurushwa wananchi na mimea yao kuharibiwa.

“Shughuli zote za matayarisho ya ujenzi kwenye ardhi hii zimeesitishwa, hadi tuwe na maafikiano kama serikali na idara ya magereza ambayo inadai kuwa wamiliki.Serikali ya Wakujaa itahakikisha haki ya Kila mwananchi imelindwa.”amesema

Wananchi wa eneo hilo hata hivyo wameitaka Serikali ya Kaunti kufuatilia na kutafuta suluhu kwa ardhi zote zenye utata kwenye Kaunti,swala ambalo waziri Elizabeth ametoa hakikisho la kuyashughulikia.

Via TaitaTaveta County Government

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours