Shida ilianza pale Jumwa ambaye alikuwa akihutubia mkutano huko Kilifi alidokeza kurejea katika baraza la mawaziri la Ruto baada ya kuundwa upya.
Umati huo uliweka wazi kuwa wale ambao tayari wametupwa nje ya baraza la mawaziri hawapaswi kurejeshwa.
“Rais William Ruto anajua na ikiwa itampendeza aseme Aisha Jumwa awe katika baraza la mawaziri na aendelee sisi watu wa Kilifi tunasema ni amina. Na akisema Aisha Jumwa apumzike tutasema ni amina” Alisema
Ni wakati huu ambapo kelele za kukataa zilizuka, na kuzima sauti yake huku umati ukiweka wazi kuwa yeye ni sehemu ya wale waliokataliwa na Wakenya na hafai kurejeshwa.
+ There are no comments
Add yours