AL-SHABAAB WAUA WANAJESHI 54 RAIA WA UGANDA

Estimated read time 1 min read

Takriban wanajeshi 54 wa Uganda akiwemo kamanda mmoja waliuawa na al-shabaab wakati wa shambulizi nchini Somalia wiki moja iliyopita, Rais Yoweri Museveni amethibitisha.

Hii ni baada ya magaidi hao kushambulia kambi ya walinda amani wa Umoja wa Afrika huko Bulamarer, kilomita 130 kusini magharibi mwa Mogadishu.

Museveni katika taarifa yake Jumamosi pia alisema kuwa makamanda wawili ambao ‘walifanya makosa’ wamekamatwa na watakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Martial.

Wiki iliyopita Museveni alisema kumetokea vifo vya Waganda lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu Wanajeshi hao wanaohudumu katika Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika Nchini Somalia (ATMIS).

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours