David Sakayo Kaluhana; ni baba mwenye umri wa miaka 62 kutoka nchi ya Kenya ambaye ameibua mshangao baada ya kuthibitisha kuwa na watoto 107 na wake 15 huku akitaka kuongeza wake wafike 1000.
David almaarufu Genius ambaye role modal wake ni Nabii Suleimani anapatikana katika kijiji kimoja huko Magharibi mwa Kenya ambapo anasema kuwa, katika ukoo wao, kila baada ya karne tatu hutokea mtu kama yeye ambaye huoa wake wengi na kupata watoto wengi.
“Akili yangu ni kubwa sana, haiwezi kubebwa na bibi (mke) mmoja, akili yangu na bibi mmoja haviwezani, lakini kuwa na wake wengi unatakiwa kuwa na akili kubwa kwa sababu ukiwa huna akili kubwa hutaweza kuwa-control,” anasema David katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga ya mtandaoni cha Afrimax.
“Kichwa kama hiki changu hakiwezi kubebwa na mwanamke mmoja, kwa sababu kina mzigo ambao yeye peke yake hawezi kuubeba. Ndio maana nilioa wake wengi. Maana nina akili sana kwa mwanamke mmoja,” Alisema Kaluhana.
Mantiki hiyo inaonekana bado inauzwa katika ujirani wake, kwa kuwa video hiyo inasema Kaluhana anaendelea kuwakumbusha wake zake kwamba wangekuwa wengi zaidi. Kaluhana anasema yeye ni kama Sulemani – mfalme wa Israeli ya kale aliyetajwa katika Agano la Kale – ambaye alikuwa na “jumla ya wake 1000”.
“Kwa mfano; Malkia wa Ethiopia Queen of Sheba aliposikia habari za Suleimani ilibidi amfuate hivyo wanawake wanapaswa kuja kwangu kwa sababu ni kama Suleimani.
Baadhi ya wake zake – Jessica, Dorin, Rose – wanasema kwenye video kwamba hawakuwahi kuwa na wivu kwa muda mrefu kuhusu wake wapya kwa sababu anagawanya wakati wake sawa kwa wote.
“Tunaishi maisha mazuri, tunapendana,” anasema mmoja wa wake hao, Rose David Kaluhana ambaye amezaa naye watoto 15.
Kuhusu kipato; David ni mwanahistoria, anaalikwa kwenye nchi mbalimbali kama Sudan, Uganda, Kongo na kwingineko kwa ajili ya kusimulia historia ya vitu vya kali na huko hujipatia kipato kinachomuwezesha kuendesha familia yake hiyo kubwa.
Kuhusu upendo kwa wake zake; David anasema wake zake wanapendana mno na wanashirikiana katika kazi na kufanikisha maendeleo ya familia kwani kila mmoja anaishi kwenye nyumba yake, lakini hushikiana katika shughuli zote kuanzia kupika, usafi na kazi za shamba na nyinginezo za kujiingizia kipato.
Filamu hiyo ina maoni zaidi ya laki 2.6 ndani ya siku mbili, na katika sehemu ya maoni kulikuwa na mchanganyiko wa ajabu na hasira. “Nashangaa kama anajua majina ya watoto wake wote …
+ There are no comments
Add yours