Baraza la mawaziri limeonya kuwa huenda kimbunga Hidaya kikalikumba eneo la pwani iwapo mvua itaendelea kunyesha.
Hii ni kulingana na taarifa iliyotelewa na baraza la maziri ambalo limesema kuwa ukanda wa pwani huenda ikakumbwa na Kimbunga Hidaya, ambacho kitasababisha mvua kubwa na mawimbi makubwa.
Taarifa hiyo pia imesema Hidaya itaambatana na upepo mkali ambao unaweza kuathiri shughuli za baharini katika Bahari ya Hindi.
Katika kipindi hicho, ngurumo za radi zinatarajiwa na mvua kali.
Takriban watu 188 wamepoteza maisha kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini.
Idara ya Met ilikuwa imesema Kenya bado itapokea mvua zaidi katika wiki zijazo.
+ There are no comments
Add yours