Wasanii Mbosso, Whozu na Billnass wametozwa faini ya milioni tatu kila mmoja na kufungiwa kutokujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo November 04, 2023 kutokana na Wasanii hao kushirikishwa kwenye wimbo wa ‘Ameyatimba’ ya Whozu , ambao maudhui yake yanatajwa kukiuka kanuni za maadili.
Baraza la Sanaa Tanzania, BASATA katika taarifa lilimtaka msanii Whozu, ambaye ndiye mwenye wimbo huo ambaye aliwashirikisha Mbosso na Billnass kwenye remix, kufuta wimbo huo mara moja kutoka kwenye majukwaa yote ya kidijitali ya kusambaza muziki.
Watatu hao waliingia studio mapema wiki jana na kufanya remix ya Ameyatimba na kuachia video yake ambayo sasa imetajwa kuwa chafu na BASATA.
Kando na marufuku ya kutojihusisha na muziki kwa miezi mitatu, watatu hao pia kila mmoja alitakiwa kulipa fiani ya shilingi milioni 3 za kitanzania.
+ There are no comments
Add yours