Mwanamuziki Beyoncé leo Ijumaa anatarajiwa kutumbuiza katika mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris huko Texas ikiwa ni siku 11 kabla ya kufanyika uchaguzi wa nchi hiyo tarehe 5 Novemba.
Kwenye hafla mbalimbali za kampeni, Harris amewahi kuonekana akicheza wimbo wa Beyoncé uitwao ‘Freedom’ lakini Beyonce hakuwahi kushiriki kwenye kampeni zake.
Beyoncé ana historia ya kuwaunga mkono wagombea Urais wa chama cha Democrat, itakumbukwa mwaka 2016 alitumbuiza pamoja na mumewe Jay-Z kwenye mkutano wa hadhara wa Hillary Clinton.
+ There are no comments
Add yours