Baada ya kuthibitishwa kuwa Director maarufu wa video mbalimbali ikiwemo za Wasanii wa Bongofleva ambaye pia ni Mtoto wa kwanza wa Muhubiri maarufu wa Arusha wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Dr. GeorDavie, Nic Davie maarufu Nisher amefariki.
Kupitia akaunti yao ya Instagram iliyothibitishwa, wameandika: “Familia ya Nabii Dk. Geordavie inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Nic Davie (Nisher) kilichotokea majira ya saa 2:08 asubuhi ya leo.
Marehemu Nisher alipata umaarufu baada ya kutengeneza video za nyimbo zilizovuma kama vile Jikubali ya Ben Pol pamoja na video kadhaa za wasanii wengi wa Bongo Flavour.
#RIPNISHER.
+ There are no comments
Add yours