Bunge Launda Kamati Ya Kuchunguza Kuondolewa Kwa Waziri Linturi

Estimated read time 1 min read

Bunge la Kitaifa limeunda wanachama wa kamati ya watu 11 iliyotwikwa jukumu la kuchunguza kuondolewa kwa Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo Mithika Linturi.

Bunge lilimteua TJ Kajwang, Yusuf Farah, Robert Mbui, na Naomi Waqo kuwa wanachama wa kamati hiyo.

Wajumbe wengine wa Kamati hiyo yenye wajumbe 11 ni Rachel Nyamai, Samuel Chepkonga, George Gitonga, Jane Njeri Maina, Kassim Sawa Tandaza, Moses Malulu, na Catherine Omanyo.

Hoja ya kumshtaki CS Linturi ilitokana na kashfa ya mbolea ghushi iliyoibuka mwezi Machi.

Mapema Alhamisi, Bunge liliidhinisha hoja ya kuundwa kwa Kamati Teule ya kutathmini madai yanayomkabili CS Linturi.

Wabunge walipiga kura kuendelea na mchakato wa kumtimua CS Linturi. Bunge liko mbioni kujadili na kuhitimisha hoja ya kumuondoa madarakani kabla ya mapumziko yake mwezi Juni.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours