CAF Yaonesha Mashaka Ya Viwanja Vya Kenya Kutumika Kwa Michuano Ya CHAN

Estimated read time 1 min read

Wakaguzi wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) wameonesha mashaka kuhusu utayari wa viwanja vya Kenya vya Kasarani na Nyayo kutumika kwa michuano ya CHAN inayotarajiwa kuanza Februari 1, 2025.

Uganda na Tanzania zote zina viwanja vilivyopitishwa na CAF, lakini Kenya bado hawana.

Kasarani Canopy imekamilika kwa 40% na mfumo wa sauti 10% wakati uwanja mzima umekamilika kwa 71%. ▪️ Uganda na Tanzania tayari wana kamati za mandalizi; na kwa upande wa Kenya bado kamati hiyo haijazinduliwa.

Viwanja vya Police Sacco, na Annex bado vinahitaji vyumba vipya vya kubadilishia nguo.

Tutarajie nini iwapo Kenya haitakidhi vigezo ifikapo tarehe 31 Desemba?

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours