Daddy Yankee, mfalme wa reggaeton, ametangaza kuwa atakuwa na mwaka mpya kama mtu single baada ya yeye na mke wake Mireddys González kuachana baada ya maisha ya ndoa kwa miaka 29. Kwenye taarifa aliyoshea kupitia Instagram Stories, Daddy Yankee, ambaye jina lake halisi ni Ramón Luis Ayala Rodríguz alisema:
“Kwa moyo uliojaa heshima na uaminifu, ninataka kushea habari muhimu kuhusu maisha yangu binafsi. Baada ya ndoa ya zaidi ya miongo miwili na baada ya miezi mingi ya kujaribu kuokoa ndoa yetu, mimi na mke wangu tunashirikiana, leo wanasheria wangu walijibu ombi la talaka lililopokelewa kutoka kwa Mireddys.”
Rapa huyo wa “Gasolina”, ambaye alistaafu kucheza mwaka jana ili kuweka upya maisha yake kwa imani yake ya Kikristo, alitangaza mgawanyiko huo Jumatatu kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Daddy Yankee, mwenye umri wa miaka 48, ambaye alifunga ndoa na González mwaka 1995 wakiwa na umri wa miaka 17, alisema kuwa imani yake itakuwa mwongozo wa kudumu wakati wa mchakato wa talaka. Alisema, “Ninaheshimu uamuzi wa Mireddys. Ninathamini wakati tulioshirikiana, uliojaa baraka na maadili, upendo na familia nzuri ambayo itaendelea kuwa kipaumbele chetu. Huu si wakati rahisi, lakini nahisi ni sehemu ya mchakato wa maisha yangu.”
+ There are no comments
Add yours