Barabara kuu ya Mombasa Malindi kwa sasa haipitiki baada ya sehemu ya daraja la Mbogolo kusombwa na mafuriko Jumamosi asubuhi.
Barabara hiyo ilikatika kabisa baada ya mafuriko kuharibu barabara ya Malindi Mombasa.
Mbunge wa kata ya Mnarani Juma Chengo alimlaumu mkandarasi anayekarabati barabara kuu kwa kuziba njia za maji na kupunguza mkondo wa mto unaozuia mtiririko wa maji.
Madereva wa Matatu wanaotumia njia hiyo wamesema hali hiyo imewaathiri kwa kuwalipia gharama za abiria wao kupanda magari mengine kuelekea wanakokwenda mara wafikapo.
+ There are no comments
Add yours