Boss wa lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz ametangaza kumtambulisha msanii mwingine mkubwa katika lebo hiyo kabla ya mwezi huu wa Novemba kukamilika.
Kupitia ukurasa wake wa X, Diamond alitoa tangazo hilo kwa maneno machache akiandika pia tarehe ambazo msanii huyo atazinduliwa rasmi katika sherehe kubwa itakayochukua siku mbili kumtambulisha.
Aprili 2020 mpaka leo kimepita kipindi cha Miaka mitatu na miezi takribani saba. Siku ambayo lebo ya muziki WCB Wasafi ilimtambulisha Zuchu, msanii mahiri wa muziki Bongo.
Muda huo umetosha kumpika msanii mpya ajaye ambapo mmiliki na mwanzilishi wa leo hiyo, Diamond Platnumz kuamua kutangaza kupitia X ujio wa staa mpya kwenye game mwezi Novemba.
+ There are no comments
Add yours