Diamond Platnumz Aeleza Kwanini Anaonekana Kumpendelea Naseeb Junior

Estimated read time 1 min read

Hivi karibuni waandishi wa habari nchini Kenya waliweza kumhoji boss wa Wasafi, Diamond Platnumz, alipokuwa ziara zake za kutumbuiza Nairobi. Aliulizwa kuhusu watoto wake, akasema kwamba wote wanaishi na mama zao. Pia alisema kuwa yeye hutumia muda wake pamoja nao wakati wowote anapoweza.

Hata hivyo Diamond aliweza kufunguka kuwa anampendelea mwanawe mdogo, Naseeb Junior, kuliko watoto wake wengine. Diamond alisema anawatendea watoto wake wote haki sawa, lakini pia alikiri kuwa hutumia muda mwingi na Naseeb Junior kwa sababu yeye ndiye mdogo.

Diamond mara nyingi ameonyesha upendo mkubwa kwa mvulana huyo mdogo aliyempata na mwanamuziki wa Kenya Tanasha Donna. Wawili hao walichumbiana kwa muda mfupi kabla ya kutengana mwaka wa 2019.

Naseeb Junior anatabiriwa kuwa mrithi anayependekezwa wa mwimbaji huyo tajiri maarufu kutoka Kigoma, Tanzania. Mama yake, Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote hata alidokeza kuhusu hilo mwaka jana.

Mwezi Desemba, Mama Dangote  aliweka wazi kuwa Naseeb ndiye mrithi rasmi wa Diamond katika biashara ya Wasafi.

Mama Dangote ya Diamond akiwa na mwanawe huyo na kusema kuwa amemkabidhi kijiti cha kuwa mrithi wake.

Mr. Tom kaka mdogo leo namkabidhi kijiti cha wasafi 👬Mimi mwenyewe,” Mama Dangote alitangaza bayana.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours