Diamond Platnumz, Akosa Kwenye Orodha Ya Wasanii Wa Tuzo Za BET Ukiwa Ni Mwaka Wa Pili Mfululizo.

Estimated read time 1 min read

Msanii wa Bongofleva na ambaye pia ni mdosi wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz, kwa mara nyingine tena ametoswa kwenye tuzo za BET ukiwa ni mwaka wa pili mfululizo!.

Tuzo hizi zinaandaliwa na Black Entertainment Television (BET) toka Juni 19, 2001 zinalenga kusheherekea mafanikio ya kazi za Wamarekani Weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji na michezo.

Ikumbukwe Diamond ndiye msanii wa kwanza Bongo kuchaguliwa kuwania tuzo za BET katika kipengele Best International Act, tayari amewania mara tatu (2014, 2016 & 2021) na kumfanya kuwa msanii pekee aliyewania mara nyingi.

Hata hivyo, katika orodha ya majina yaliyotoka hapo jana, jina la Diamond halipo licha ya mwaka uliopita kufanya vizuri na album yake, First of All (FOA) iliyotoka Machi 2022 ikiwa na nyimbo 10.

Katika kipengele cha Best International Act ambacho Diamond amekuwa akiwania miaka yote, kuna Burna Boy, Ayra Starr (Nigeria), KO (Afrika Kusini) n.k.

Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa Juni 25, 2023 katika ukumbi wa Microsoft Theater Jijini Los Angeles, Marekani.

Ikumbukwe Eddy Kenzo toka Uganda ndiye msanii wa kwanza Afrika Mashariki kushinda tuzo ya BET, mwaka 2015 aliibuka mshindi katika kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act, huku Rayvanny akishikilia rekodi upande wa Tanzania ambapo mwaka 2017 alishinda katika kipengele hicho pia.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours