Boss wa Wasafi, Diamond Platinumz amefunguka kutapeliwa zaidi ya Billion Nne.Kupitia mahojiano yake na wanahabari.
Diamond amesema kwamba mipango yake ilivurugika baada ya kutapeliwa.
“Mimi nilikuwa nimenunua [ndege] kubwa ya kwangu ila wakaniletea ujanja wakaniingiza mjini kidogo wakanipiga kama bilioni 4 na kitu. Polisi wanafahamu na inaendelea kufuatiliwa na serikali wananisaidia kuona haki yangu naipata aje,” Diamond Platinumz.
Msanii huyo alisema kwamba ameshaanza kurudishiwa kidogo hela hizo na anaamini mwisho wa siku atapokea hela zake zote ili kuendelea na ndoto yake ya kumiliki ndege.
Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii barani Afrika ambao usafiri na vifaa vya bei ghali zikiwemo ndege za kibnafsi na magari ya dhamani ya juu wakati anapozuru taifa lolote kufanya tamasha la muziki.
+ There are no comments
Add yours