Baada ya familia kutoa ilani kwa vyombo vya habari,madjs na yeyote yule kucheza ngoma za mwendazake Ally B ambaye aliweza kustiriwa jana 2 Novemba,hisia mseto zinazidi kuibuka kutoka kwa mashabiki.
Kakake Ally B alitoa ombi la unyenyekevu kwa niaba ya familia kwa vituo vya redio na watumbuizaji kuacha kucheza nyimbo zake kufuatia kifo chake.
“Tunaomba news anchors, radio presenters, ma-dj, tafadhali naomba, nyimbo za Ally msicheze. Tafadhali naomba,” Kakake Ally B’s alisema.
Alieleza kuwa walitaka roho ya mwimbaji huyo ipumzike kwa amani na kuwataka wanaotaka kuendelea kumsherehekea badala yake wamuombee.
“Msicheze miziki yake tena. Naomba iwe anayetaka akimkumbuka amtilie dua. Lakini msipige miziki yake, tafadhali. Twaomba,” Alisema.
“Nyimbo zake tosha. Muombeeni lakini msipige miziki yake. Mimi kama ndugu yake nimesema,”.
+ There are no comments
Add yours