Simba SC imefungiwa kufanya usajili hadi pale itakapoilipa timu ya Teungueth aliyokuwa akichezea kiungo Pape Ousmane Sakho.
–
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) imeeleza kuwa uamuzi huo umetolewa na FIFA baada ya klabu hiyo kushinda kesi dhidi ya Simba kuhusu mauzo ya Sakho.
–
Taarifa hiyo imeeleza Teungueth ilifungua kesi kudai malipo ya mauzo ya Sakho, ambapo Simba ilitakiwa kukamilisha deni hilo kwa siku 45 tangu ilipoamuliwa hivyo na FIFA lakini haikufanya hivyo.
–
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kama kanuni zinavyoeleza, wakati FIFA ikiweka marufuku ya usajili wa kimataifa, TFF pia imeweka marufuku ya usajili wachezaji wa ndani.
–
Imeandaliwa na Rahim Fadhil
Umejisajili #MwangwiwaUkarimu #EchoesofKindness
+ There are no comments
Add yours