Gavana anayeondoka wa Mombasa Hassan Joho na Gavana Teule wa Abdullswamad Shariff Nassir wapeana haki miliki ya Ardhi kwa wakazi wa Likoni Block 203
kupitia mtandao wa facebook Hassan joho alisema ilikuwa baadhi ya mipango ya serikali ya kuhakikisha wakazi wa Mombasa wamepata hati miliki ya mashamba.
“Baada ya miongo kadhaa ya kupigania haki ya ardhi watu wa Likoni Block 203 wanayo leo kuwa wamiliki wa ardhi. Niliandamana na Gavana mteule Mh. Abdullswamad Shariff Nassir na uongozi wa Mombasa nilipowasilisha Hati Miliki zaidi ya 1000 kwa wakazi wa Mrima, Msufini, Maweni, Mathare na BwagaBwaga. Hili liliwezeshwa na ushirikiano kati ya Benki ya Dunia, serikali ya kitaifa na kaunti ya Mombasa na jamii ya wenyeji katika kufanikisha mpango wa KISIP”
+ There are no comments
Add yours