Gavana wa Taita Taveta Andrew Mwadime Wakujaa, akiandamana na naibu wake Mh.Christine Kilalo pamoja na Kamishna wa Kaunti Bi.Josephine Onunga, hii Leo wameongoza wananchi wa Kaunti kwa sherehe za Jamhuri,mjini Voi.
Akiongea mjini Voi,Gavana Wakujaa ameisuta bodi ya kusimamia maji pwani,kwa kusitisha huduma za maji Kaunti ya TaitaTaveta kwa sababu ya deni la kihistoria la kuanzia mwaka 2006, huku akiwataka wabunge wa pwani washirikiane na kuwasilisha hoja bungeni ya kubadilisha sheria,ili Kaunti zianze kusimamia raslimali ya maji.
“Hatuwezi sema tuko huru wakati tunaendelea kupitia dhuluma kama hizi.Kama Gavana wa Jimbo hili katu sitokubali wananchi wangu waendelee kupitia dhuluma hiii”.
Kuhusu janga la mafuriko ,Wakujaa ametoa hakikisho kwa wananchi wote hususan walioathiriwa na mafuriko kuwa serikali yake inashirikiana na wahisani mbalimbali kuhakikisha walioathiriwa na mafuriko wamesaidiwa kurejelea maisha yao ya kawaida,huku akitoa tahadhari kwa wananchi walio kwenye sehemu ambazo huathiriwa na mafuriko wahamie maeneo salama,ikizingatiwa idara ya utabiri wa Hali ya anga imetabiri mvua itaendelea kunyesha kwa wingi.
Wakujaa aidha alitumia fursa hii kuweka wazi miradi mbali mbali ambayo serikali yake imetekeleza kuanzia kitengo cha afya,elimu,kilimo,Madini,miongozi mwa sekta zingine.
“Japo kuna changamoto mbalimbali ambazo zinaambatana na maswala ya uongozi, serikali yangu imeweka misingi yote mhimu ya kuhakikisha mwananchi anaendelea kupata huduma zote mhimu”.ameeleza
Bi Kilalo kwa upande wake amesistiza umuhimu wa Kila mmoja kutambua kua uhuru unapiganiwa siku baada ya siku, ili kufanikisha maendeleo ya Kaunti na taifa kwa jumla
“Kama viongozi wenu wa Kaunti mliotuchagua tutaendelea kusukuma haki ya Kila mmoja izingatiwe pasi na kujali iwapo uwezo au nafasi mtu anashikilia kwa jamii, hususan haki ya Ardhi”.amesema.
Mbunge wa Voi Abdi Chome, viongozi wa utawala ,mawaziri wa Kaunti ,maafisaa wakuu wa Kaunti walihudhuria sherehe hizo
+ There are no comments
Add yours