Chelsea ilipoteza uongozi na kupata sare ya 1 – 1 dhidi ya Crystal Palace uwanjani Stamford Bridge Jumapili.
Nicolas Jackson aliwatanguliza Chelsea dakika ya 25 baada ya Noni Madueke kumpa pasi Cole Palmer aliyemwandaa Jackson kwa bao hilo.
Hata hivyo, Palace walisawazisha dakika ya 53 wakati Eberechi Eze alipotuma tobwe lililomshinda kipa Robert Sanchez kuzuia.
Chelsea wanakalia nambari ya 11 na alama nne. Palace kwa upande wao wako nafasi ya 16 na alama moja.
+ There are no comments
Add yours