Msanii nguli wa bongo Harmonize Ambaye kwa Sasa Yupo Nchini Marekani Ametangaza kufanya maandamano Baada ya kushinda TUZO Tatu Mfululizo.
Kupitia insta story yake Ameandika haya
“Tangu muziki wetu au niseme SANAA yetu ianze, SIKUMBUKI lini mara ya mwisho msanii kutoka Tanzania kulipatia hili Taifa la mama samia tuzo Tatu (3) za kimataifa ndani ya usiku mmoilja.! Moja au mbili, Nakumbuka ila Tatu sina kumbukumbu kwahiyo paledi litaanzia airport mpaka KONDE VILLAGE alafu tunakesha mpaka asubuhi, soon nawarudia na Tarehe pamoja na saa ninayotua
Harmonize ameshinda tuzo hizo mbele ya mastaa mbalimbali wakiwemo mastaa kutoka Nigeria.
Miongoni mwa wasanii waliokuwa kwenye kipengele kimoja na @harmonize_tz ni pamoja na Burna Boy, Davido, Asake na wengine
+ There are no comments
Add yours