Jada Pinkett Smith Asema Yeye na Will Smith Walitengana Tangu 2016

Estimated read time 1 min read

Muigizaji na mtangazaji Jada Pinkett Smith amefichua kuwa yeye na mumewe Will Smith wamekuwa wakiishi “maisha tofauti kabisa” tangu 2016.

Jada ameweka wazi kuwa ingawa wawili hao wamekuwa wakiishi maisha tofauti kabisa kwa miaka saba na hawakuwa tayari kuthibitisha hadharani.

Katika mahojiano na kituo cha NBC Jada amekiri kuwa yeye na mumewe bado wanaishi tofauti, lakini hawana mpango wa kupeana talaka.

Kulikuwa na uvumi juu ya ndoa yao mwaka 2020 baada ya Jada kupitia kipindi chake cha Red Table Talk kujadili ‘uhusiano’ wake na msanii August Alsina.

Itakumbukwa Will Smith aliushangaza ulimwengu baada ya kumuwamba kofi mtangazaji Chris Rock kwenye sherehe ya tuzo za Oscar 2022 baada ya mtangazaji huyo kufanya mzaha juu ya ‘upara’ kwa Jada Pinkett Smith.

Inashangaza kumuona Will Smith akighadhabika kiasi kile na kumpiga kofi Chris Rock jukwaani licha ya kwamba yeye na mkewe huyo hawako pamoja.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours