Jeshi la Burkina Faso limesema limemuondoa madarakani Rais Kabore, kusimamisha katiba, kuvunja serikali na kufunga mipaka.

Estimated read time 1 min read

Jeshi la Burkina Faso limechukua uskani wa nchi siku ya Jumatatu, na kumuondoa madarakani Rais Roch Kabore, kuvunja serikali na bunge, kusimamisha katiba na kufunga mipaka yake.

Mapinduzi hayo yalitangazwa kwenye televisheni ya taifa na Kapteni Sidsore Kader Ouedraogo, ambaye alisema jeshi limenyakua mamlaka katika kukabiliana na ‘udhalilishaji unaoendelea wa hali ya usalama’ nchini humo na serikali kutokuwa na uwezo wa kuunganisha watu.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours