Magavana wa pwani tarehe 25, Octoba waliungana eneo la pwani kwa ufunguzi rasmi wa Jengo la Ofisi ya Sekretarieti ya Go Blue JKP huko Nyali, Kaunti ya Mombasa.
Mpango wa Go Blue, uliobuniwa kwa ushirikiano na Umoja wa Ulaya na Serikali ya Kitaifa, umesaidia pande nyingi katika uchumi kwa kutoa fursa za kazi kwa vijana na wanawake katika sekta kama vile utalii na uvuvi mdogo. Mbinu hii pia itawezesha ukuaji wa kijamii na kiuchumi wa ukanda wa pwani.
Mpango wa Go Blue unaandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kaunti za Pwani na unalenga kutoa nafasi za kazi kwa vijana na wanawake katika sekta zinazowahudumia kama vile utalii, ufugaji wa samaki na uvuvi mdogomdogo. Voi VTC kupitia mradi wa Go Blue kwa sasa ni kituo cha mafunzo cha ubora ambapo idadi kubwa ya vijana wanapitia mafunzo kuhusu ujuzi wa kuajiriwa.
Mkutano ulijadili maeneo ya ushirikiano zaidi katika Uchumi wa Bluu. “Hii ni sekta ambayo tunavutiwa nayo kwa sababu itasaidia katika maendeleo ya kiuchumi ya kaunti yetu na ukanda wa pwani. Itafungua fursa nyingi za kazi kwa watu wetu,” Gavana Mwadime alisema.
Voi VTC kupitia mradi wa Go Blue kwa sasa ni kituo cha mafunzo cha ubora ambapo idadi kubwa ya vijana wanapitia mafunzo kuhusu ujuzi wa kuajiriwa.
Go Blue inafadhiliwa kwa Shilingi bilioni 3.23 za Kenya na kutekelezwa katika kaunti za pwani za Mombasa, Kwale, Kilifi, Tana River, Lamu, na Taita Taveta. Gavana Gideon Mung’aro wa Kilifi, Gavana Andrew Mwadime, Dhadho Godhana wa Tana River, Mkurugenzi Mtendaji Baraza la Magavana Bi Mary Mwiti, Jumuiya Ya Kaunti Za Pwani na mwenyeji Naibu Gavana wa Mombasa Mhe. Francis Thoya walihudhuria miongoni mwa viongozi wengine.
+ There are no comments
Add yours