Baada ya kuachana na Harmonize, Muigizaji wa Tanzania, Kajala Fridah amesema kwa sasa yupo katika penzi jipya.
Kajala ametangaza kuwa kwenye uhusiano mpya baada ya kuachana na nyota huyo wa bongo fleva. Mama huyo wa mtoto mmoja aliweka kwenye Instagram Story yake kuwa ana mwanaume mpya ambaye ameweza kumfurahisha na anafurahia uhusiano huo.
“Nimempata mwanaume niliyemtaka, sasa nina furaha.” amesema Kajala.
Hata hivyo hakufichua maelezo kuhusu mwanamume huyo mwenye bahati.
Haya yanajiri takriban mwaka mmoja tangu Kajala na Harmonize walipoachana. .
+ There are no comments
Add yours