Mh. Kalonzo Musyoka na kikosi cha Wiper party, hapo jana kilipeleka kampeni za wiper mjini Taveta.
Chama cha Wiper kinawania kushinda viti vya siasa eneo la Taitataveta, hii ni baada ya kupatiana tiketi kwa wawaniaji kuanzia ugavana hadi viti vya mca.
Miongoni wa waliokuwepo kwa mkutano huo ni mwaniaji wa ubunge kupitia chama cha Wiper Wakili Bwire, Mwaniaji wa ugavana Dan Mwazo, Mbunge wa Wundanyi Mh. Danson Mwashako na aliyekuwa naibu wa gavana na ambaye kwa sasa anawania ubunge wa Mwatate Mh. Mjala Mlaghui.
Tikiti za wiper zimevutia wawaniaji wengi kaunti ya TaitaTaveta baada ya chama hicho kushinda kiti cha ugavana na ubunge wa Wundanyi mwaka wa 2017.
Asante sana Taveta! I've really enjoyed today's interaction with the Buffalo gang. I will be back! ^SKM pic.twitter.com/hIhUcTsU4G
— Kalonzo Musyoka (@skmusyoka) May 13, 2022
+ There are no comments
Add yours