Kalonzo azuiwa kuandaa mkutano wa umma mjini Mombasa

Estimated read time 1 min read

Nyufa zinazidi kujitokeza katika muungano wa Azimio La Umoja One Kenya aliance baada ya serikali ya Mombasa kumnyima Kalonzo Musyoka kufanya mkutano wa umma kwa uwanja maarufu wa Tononoka.

Kalonzo ambaye alikuwa ziara ya kisiasa Mombasa aliandamana na aliyekuwa gavana wa Nairobi, Mike Sonko, anayekodolea macho wadhifa huo katika kaut ya Mombasa.

Gavana Joho anampigia debe mbunge wa Mvita, Abdulswamad Shariff Nassir, kuwa mrithi wake

Sonko na Nassir wanatarajiwa kuchuana kwa tickiti ya Wiper na ODM mtawalia ijapokuwa wote ni wanachama wa Azimio La Umoja One Kenya Coalition Party

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours